GRACE COMMUNION INTERNATIONAL
KANUNI YA IMANI
Utambulisho
Grace Communion International ni muungano wa washiriki kutoka pembe mbali mbali za dunia hasa nchi zenye washiriki kwa sasa ni 100. Wito wetu ni kuienzi, kushiriki na kuhubiri injili ya Yesu Kristo na kutoa msaada wa kiroho kwa washiriki wetu ili kuwalea kiroho. (Mt. Matthayo 28:19‐20)
Neno la Bwana linawasihi wakristo kukua kwa neema na uelewa wa Yesu Kristo. (2 Petro 3:18). Roho mtakatifu wa Mungu huongoza kanisa katika ukweli wote (Mt. Yohana 16:13). Ndio maana kauli hii ya imani sio kanuni ya imani iliyotamatishwa na kongamano la Grace
Communion International huifanyia mabandiliko kadri Roho wa Bwana anavyotuongoza.
Muhutsari wa imani yetu ya Kikristo.
Imani yetu ni kwa Mungu mmoja – Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Mungu Baba aliumba vitu vyote kupitia kwa Mwana na hutupatia Roho Mtakatifu kama.
Mwana wa Mungu ambaye ndiye Yesu Kristo na mwokozi wetu, alizaliwa Bikra Maria, akiwa
Mungu kamili na binadamu kamili na ndiye ufunuo wa utimilifu wa Mungu na utimilifu wa wa Binadamu katika haki. Aliumia na kufa kifo cha msalaba kwa ajili ya dhambi za wanadamu, akafufuka siku ya tatu na akainuliwa binguni. Anasimama kama kiwakilishi cha wanadamu mbele za Mungu Baba, yesu Kristo ni kiwakilishi timilifu cha wanadamu mbele za Mungu. Kwa kuwa alisulubishwa kwa ajili ya dhambi za binadamu wote, wote walikufa ndani yake, na wote watainuliwa ndani yake.
Roho mtakatifu huwaleta wenye dhambi kwenye msamaha na imani, huwadhibitishia waumini msamaha wa dhambi, na ukumbalifu wao kwa Mungu kama wanawe wapendwa, hufanya kazi ndani yao ili kuwabandilisha na kuwapa ukubali kama wa Yesu Kristo.
Biblia takatifu ni neno la ukakika kutoka kwa Mungu linalotoa ushuhuda wa Yesu Kristo. Biblia ndiyo yenye kuaminika kuhusu mambo ya imani na wokovu.
Wokovu unapatikana tu kwa neema ya Mungu na sio kwa vitendo, na unadhihilika kupitia kwa imani ndani ya Yesu Kristo. Wakisto huonyesha pendo na furaha ya wokovu huo wanapokutana pamoja mara kwa mara na wanapoishi maisha ya kiungu ndani ya Yesu Kristo.
Maono yetu ni ufufuo kutoka kwa wafu na maisha ya milele yanayokuja.
Mungu ‐ Nafsi tatu kwa moja.
Kwa ushuhuda wa maandiko matakatifu, ni mtakatifu mwenye nafsi tatu kwa pamoja, wanaishi kwa pamoja Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ila kila mmoja kwa nafsi moja. Mungu anajulikana tu kwa nafsi tatu na nafsi zote tatu zinajulikana tu kama Mungu ambaye sifa zake kuu za wema, mwenye kudura, mwenye maarifa yote na apatikanaye kila mahala na asiyebadilika katika agano lake kwa wanadamu. Ni Mungu wa muumba ya mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, yeye ndiye huhimili ulimwengu na vyote vilivyomo. Ndiye mwanzilishi wa wokovu wa mwanadamu. Japo mara kwa mara tunamsaliti katika matendo yetu, Mungu bila masharti na kwa upendo wake, neemana wema usiopimika anajuhusisha katika maisha ya wanadamu kupitia kwa njia ya Yesu Kristo ili wanadamu kwa Roho Mtakatifu waweze kuridhi na kuwa washiriki wa maisha ya milele kama wanawe wapendwa.
(Mt. Mariko 12:29; Mt. Matthayo 28:19; Mt. Yohana 14:9; 1 Yohana 4:8; Warumi 5:8; Tito 2:11; Waebrania 1:2‐3; 1 Petro 1:2; Wagalatia 3:26)
Mungu Baba
Mungu Baba ndiye nafsi ya kwanza katika nafsi tatu za Uungu, ambaye milele ndiye chimbuko la Mwana (Yesu Kristo), vile vile Roho Mtakatifu milele yote huanzia kwake na kupitia kwa Mwana. Kupitia kwa Mwana, Mungu Baba ndiye muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, kwa anjili ya wokovu wa ulimwengu, Mungu Baba alimtuma Mwana atolewe kama kafala ya dhambi za ulimwengu na hutupatia Roho Mtakatifu kwa ajili ya wongofu na kupangwa kama watoto wake.
(Mt. Yohana 1:18; Warumi 15:6; Wakolosai 1:15‐16; Mt. Yohana 3:16; 14:26; 15:26; Warumi 8:14‐17; Matendo ya Mitume 17:28)
Mungu Mwana
Mwana ndiye nafsi ya Pili katika nafsi tatu za Uungu, ambaye milele chimbuko lake ni Baba,
yeye ndiye neno na kwa ulimwengu ndiye mfano wake Baba. Kupitia kwa Mwana, Mungu Baba ndiye muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, na huvitunza vyote kwa neno. Alitumwa na Baba ili kumthihirisha katika ulimwengu kwa anjili ya wokovu wetu. Bikra Maria akambemba miimba ya Roho Mtakatifu akiwa Mungu kamili na vile vile binadamu kamili nafsi mbili katika moja. Ndiye mwana wa Mungu na mtawala wa vyote, mwenye sifa ya kuambundiwa, utukufu na mdhamini wetu. Kama mwokozi wa ulimwengu alitabiriwa, aliumia na kusurubishwa kwa anjili ya dhambi za ulimwengu, akafa, akafufuka na kuinuliwa mbinguni. Alichukua udhaifu, kutengwa kwetu na kupitia kwake wanadamu wote wameshirikishwa tena katika uhusiano kamilifu na Mungu Baba ili kupitia kwa ufufuo wake wanadamu washirikishwa kama wana wa Mungu kwa kupangwa kupitia kwa Roho mtakatifu. Kama mwakilishi wetu na anayechukua nafasi yetu, ni mwakilishi wa kila binadamu mbele za Baba, akitoa majibu kamili/yanayastahili kwa Baba kwa niamba ya wanadamu ili kutoa patanisha kati ya wanadamu na Mungu. Atarejea tena kwa utukufu akiwa Mfalme wa Wafalme juu ya ulimwengu wote.
(Mt. Yohana 1:1, 10, 14; Wakolosai 1:15‐17; Wahebrania 1:3; Mt. Yohana 3:16; Tito 2:13; Mt.Mathayo 1:20; Matendo ya Mitume 10:36; 1 Wakorintho 15:3‐4; Tito 3:4‐5; Wahebrania 2:9; 7:25; Wagalatia 4:5; 2 Wakorintho 5:14; Waefeso 1:9‐10; Wakolosai 1:20; 1 Timotheo 2:5; Wahebrania 1:8; Ufunuo wa Yohana 19:16)
Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu ndiye nafsi ya tatu katika nafsi tatu za Uungu, ambaye milele chimbuko lake ni Baba kupitia kwa Mwana (yesu Kristo). Ndiye mfariji aliye ahidiwa na Yesu Kristo, muunganishi kati ya Mungu Baba, Mwana na Wanadamu, vile vile hubadilisha wanadamu na kuwapa sura/mfano ya Yesu Kristo. Roho Mtakafifu hufanya kazi ndani yetu ili wongofu tuliopewa na Mungu kupitia kwa Mwanae Yesu Kristo utimilike kwa kuendelea kutuunda upya, kutuwezesha kushirika katika utukufu wa Mwokozi wetu, na ushirika wa milele na Baba kama wanawe. Roho Mtakatifu ndiye chanzo cha msukumo na utume kwenye maandiko yote ta Biblia, ndiye chanzo cha mshikamano na ushirika ndani ya kanisa. Ndiye anayetoa vipawa vya Roho Mtakatifu kwa anjili ya kueneza ujumbe wa Bwana na ndiye anayengoza wa Wakristo katika njia za kweli asiyebadilika.
(Mt. Mathayo 28:19; Mt. Yohana 14:16; 15:26; Matendo ya Mitume 2:38; Mt.
Mathayo 28:19; Mt. Yohana 14:17, 26; 1 Petro 1:2; Tito 3:5; 1 Wakorintho 3:16; Warumi 8:16; 2 Petro 1:21; 1 Wakorintho 12:13; 2 Wakorintho 13:14; 1 Wakorintho 12:1‐11; Mt. Yohana 16:13)
Ufalme Wa Mungu
The kingdom of God in the broadest sense is God’s supreme sovereignty. Kwa upana wake,
Ufalme wa Mungu ni dhihilisho la enzi au Ukuu wa Mungu. Utawala wa Mungu unadhihirishwa kupitia Kanisa na katika maisha binafsi ya kila Muumini anayetii na kuyafuata mapenzi yake. Ufalme wa Mungu utadhihirishwa kikamilifu katika ulimwengu atakaporudi Yesu Kristo na kukabidhi vyote kwa Mungu Baba.
(Luka 17:20‐21; 1 Wakorintho 15:24‐28; Wakolosai 1:13; Ufunuo wa Yohana 1:6; 11:15; 21:3,22‐27; 22:1‐5)
Binadamu
Mungu aliwaumba binadamu Mume na Mke katika mfano wake. Mungu akawabariki, na
kuwapa agizo la kuongezeka na kujaza ulimwengu. Kwa upendo akampa binadamu usimamizi/ukadamu wa dunia na viumbe vyote. Adamu akiwa kama mwakilishi wa wanadamu, alifanya dhambi iliyomtenga na Mungu na wanadamu wote wanaishi katika dhambi dhidi ya Mungu; hali hiyo ilieneze mateso na kifo katika ulimwengu. Pamoja na udhaifu wa wanadamu, na maisha ya dhambi, mwanadamu anaendelea kuishi na kutambulika kama kiumbe na sura ya Mungu. Kwa hayo yote wanadamu wote kwa ujumla wao na kama mmoja mmoja wanastahili kupendwa, kuheshimiwa na kuzingatiwa. Yesu Kristo ambaye ndiye Adamu wa mwisho ndiye sura timilifu ya Mwenyezi Mungu. Mungu kupitia kwa Yesu Kristo anaumba upya binadamu ambaye dhambi na kifo havitakuwa na uwezo juu yake. Ndani ya Yesu, wanadamu wanapokea sura timilifu ya Mungu, na kuungana na Yesu Kristo wanadamu wanashirikishwa katika uhusiano timilifu walionao Mungu na Yesu Kristo.
(Mwanzo 1:26‐28; Warumi 5:12‐21; Wakolosai 1:15; 2 Wakorintho 5:17; 3:18; Warumi 8:29; 1 Wakorintho 15:21‐22; 47‐49; 1 Yohana 3:2; Wakolosai 3:3‐4)
Maandiko Matakatifu
Maandiko matakatifu kupitia kwa neema ya Mungu yametakaswa na kufanya takatifu ili
kuhudumu kama kariha/zinduko kutoka kwa Mungu na vile vile yawe shuhuda aminifu kwa
Yesu Kristo na injili. They are the fully reliable record of God’s revelation to humanity
culminating in his self‐revelation in the incarnate Son. Kwa hali hiyo, maandiko matakatifu ndo msingi bora kwa kanisa na yenye hakika katika mambo yote ya imani na wokovu.
(2 Timotheo 3:15‐17; 2 Petro 1:20‐21; Yohana 5:39; 17:17)
Kanisa
Kanisa ambalo ndio mwili wa Kristo ni mkusanyiko wa wote wanaoamini katika Kristo. Kanisa imepewa agizo/mamlaka kuandaa wafuasi wa Yesu na kwa upendo kuwatafuta, kuwatunza na kuwabatiza wanaoamini kufuata na kutunza maagizo yote ya Yesu. Katika kutekeleza agizo hilo, kanisa linelekezwa na maandiko matakatifu, kwa maelekezo ya Roho Mtakatifu ambaye anaishi ndani ya wakristo, na kila mara huangalia msaada wa Yesu Kristo kama kiongozi aishie kama kiongozi wao.
(1 Wakorintho 12:13; Warumi 8:9; Mt. Matthayo 28:19‐20; Wakolosai 1:18; Waefeso 1:22)
Wakristo.
Mkristo ni mtu yeyote anayeamini na kufuata maagizo ya Yesu Kristo. Wakristo wanazaliwa
mara ya pili baad aya kuongolewa na Roho Mtakatifu, wanakumbatia kupangwa kwao kama
wana wa Mungu na kuingia katika uhusiano wa kweli na Mungu na wanadamu wenzao kupitia kwa neema ya Mungu na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Wakristo wanajulikana kwa matunda ya Roho Mtakatifu.
(Warumi 10:9‐13; Wagalatia 2:20; Mt. Yohana 3:5‐7; Tito 3:5; Mt. Mariko 8:34; Mt. Yohana 1:12‐13; 3:16‐17; Warumi 5:1; Warumi 8:9, 14‐15; Mt. Yohana 13:35; Wagalatia 5:22‐23)
Injili Takatifu.
Injili Takatifu ndio habari njema ya ufalme wa Mungu na wakovu wa Mungu kwa neema ya
Mungu kupitia kwa imani ndani ya Kristo. Ndio ujumbe wa kweli kuwa Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi na kwa tendo hilo ametufanya wake hata kabla yetu kuamini katika ndani yeye na ametuunganisha naye kwa upendo na kutuhakikishia kuwa daima hatatuacha. Kwa hali hiyo, anaita wanadamu wote ili watumbu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wao.
(1 Wakorintho 15:1‐5; Wakolosai 2;13: 1 Yohana 2:2; Warumi 5:8, 18‐21; Mt. Yahona 3:16‐17; Mt. Luka 24:46‐48; Wakolosai 1:19‐23; Matendo ya Mitume 8:12; Mt. Matthayo 28:19‐20)
Mwenendo wa Wakristo.
Mwenendo wa Mkristo unatambulika kama maisha ya imani na utii wa dhati kwa Yesu Kristo
ambaye alitupenda na akatoa maisha yake kwa ajili yetu. Imani katika Yesu inajidhihilisha kwa kuamini injili na kushiriki katika kazi ya upendo wa Yesu Kristo. Kupitia kwa Roho Mtakatifu, Yesu Kristo anabadili mioyo ya waumini ili kudhihirisha upendo, furaha, amani, uaminifu, unyenyekevu, huruma, wema, upole, uwezo wa kudhibiti nafsi, uadilifu na ukweli. (1 Yohana 3:16, 23‐24; 4:20‐21; 2 Wakorintho 5:15; Waefeso 2:10; Wagalatia 5:6, 22‐23; Waefeso 5:9)
Neema ya Mungu
Mungu anatupatia neema yake bure hata bila sisi kustahili na inadhibitika kwetu kwa yote
ayafanyayo kwetu. Kwa neema Mungu aliuokoa ulimwengu na wanadamu kutoka kwenye
minyororo ya dhambi na hukumu ya kifokupitia kwa mwanae Yesu Kristo, vile vile, kwa neema, Roho Mtakatifu anawezesha wanadamu kumjua na kumpenda Mungu na Yesu Kristo na kwa hali hiyo wanadamu wanapata uzoefu wa furaha ya wokovu katika ufalme wa Mungu.
(Waefeso 2:8‐9; 1 Yohana 2:1‐2; Wakolosai 1:20; Warumi 11:32; 8:19‐21; 3:24; 5:2, 15‐17, 21; Mt. Yohana 1:12; Tito 3:7)
Dhambi
Dhambi ni hali inayotenganisha wanadamu na Mungu na kwa ujumla wake inatokana na
kitendo chochote kilicho kinyume na mapenzi ya Mungu kama vile makosa, kutotenda wemama kutoamini katika neema ya Mungu na upendo wake unaojidhihilisha kupitia kwa Yesu Kristo. Biblia inahusisha dhambi na Shetani ambaye kazi zake alikuja kuziharibu Yesu Kristo. Matunda ya dhambi ni kuharibu mahusiano, mateso na kifo. Kwa kuwa wanadamu wote ni wadhambi, wakristo wote wanahitaji habari njema kuwa Mungu anawapenda bila masharti, amewasamehe dhambi zao na kuwarejesha kwake kupitia kwa mwanae Yesu Kristo.
(1 Yohana 3:4; Yakobo 4:17; Warumi 14:23; Warumi 5:12, 17‐19; 7:24‐25; Mt. Mariko 7:21‐23; 1 Yohana 3:8; Waefeso 2:2; Wagalatia 5:19‐21; Warumi 6:23; 3:23‐24; Waefeso 2:12‐13)
Imani katika Mungu
Imani katika Mungu ni zawadi kutoka kwa Mungu, ambayo kiini chake ni Yesu Kristo na
inabainishwa kwa ushahidi wa Roho Mtakatifu katika maandiko. Kwa imani, Mungu anaadaa na kuwezesha nafsi yetu kushiriki katika ushirika wa Yesu Kristo, Mungu na Roho Mtakatifu. Yesu ndiye mwazilishi na mfanikishaji wa imani yetu.
(Waefeso 2:8; Warumi 12:3; Warumi 10:17; Wahebrania 11:1; Warumi 5:1‐2; 1:17; 3:21‐28; 11:6; Waefeso 3:12; 1 Wakorintho 2:5; Wahebrania 12:2) Wokovu
Salvation
Wokovu ni urejesho wa uhusiano kati ya wanadamu na Mungu na ukombozi wa viumbe vyote kutoka kwenye utumwa ya dhambi na kifo. Wokovu unapatikana kwa neema ya Mungu na unadhihirika kupitia kwa imani katika Yesu Kristo, haupatikani kutokana na wema wetu au matendo mema. Mungu anaita kila binadamu kuingia kwenye ushirika mtakatifu, ambao tumehakikishiwa na Yesu Kristo na tumeunganishwa naye kama wapendwa wa Mungu kwenye mkono wa kuume wa Mungu.
(Warumi 8:21‐23; 6:18, 22‐23; 1 Wakorintho 1:9; 1 Timotheo 2:3‐6; Mt. Mathayo 3:17; Wakolosai 3:1; Waefeso 2:4‐10)
Toba
Toba kwa Mungu ni badiliko la mawazo na mtazamo/fikra kwa kuitikia wito wa neema ya
Mungu kwa kuchochewa na Roho Mtakatifu na kwa misingi ya neno la Mungu. Toba inahusu
utambuzi wa dhambi binafsi na imani kwa na utii kwa Yesu Kristo ambaye kupitia kwake
wanadamu wote wamepatanishwa na Mungu na kupata maisha mapya yaliyotakaswa na Roho Mtakatifu kupitia kwa imani katika Yesu Kristo.
(Matendo ya Mitume 2:38; 2 Wakorintho 5:18‐19; Warumi 2:4; 10:17; Wakolosai 1:19‐20; Warumi 12:2)
Ubatizo
Sakaramenti ya ubatizo ina bainisha kuwa tunaokolewa na Yesu Kristo pekee na sio kutokana na kutumbu au imani yetu. Sakaramenti hii ni kuonyesha kushiriki kwa muumini katika kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, ambapo maisha yake ya awali yanasurubishwa na kuyakataa ndani ya Yesu. Vile vile pingu za maisha ya kale zilizokuwa kizuizi cha mahusiano kamilifu kati ya muumini na Mungu zinakatika kupitia ufufo wa Yesu Kisto. Ubatizo unatangaza neno njema kuwa Kristo ametufanya wake, na ni kupitia kwake tu maisha yetu mapya ya imani na utii yanachimbukia. Ushirika wa Grace Communion International tunabatiza kwa kuzamisha kwenye maji.
(Warumi 6:3‐6; wagalatia 3:26; Wakolosai 2:12; Matendo ya Mitume 2:38)
Meza ya Bwana
Katika Sakramenti ya meza ya Bwana tunashiriki mkate na divai kama ukumbusho wa mwokozi wetu, tukitangaza kufa kwake mpaka atakaporudi. Meza ya Bwana ni kushiriki katika kifo na ufufo wa mwokozi wetu. Kama mkate na divai ilivyowakilisha miili yetu, vivyo hivyo kwa neema tunashiriki kiroho katika mwili na damu ya Yesu Kristo. Kwa hali hiyo meza ya Bwana inaashiria kwa waumini kuwa katika kila sehemu ya maish yetu, hatutegemei uaminifu au utakatifu wetu bali ni kwa neema za Mungu tunapata ukubali wa Mungu kupitia kwa Yesu Kristo.
(1 Wakorintho 11:23‐26; 10:16; Mt. Matthayo 26:26‐28; 1 Wakorintho 1:9; 2 Timotheo 1:9)
Kuja kwa Yesu Mara ya Pili.
Kama alivyoahidi Yesu Kristo, atarudi mara ya pili kuhukumu na kutawala dunia yote kwenye
Ufalme wa Mungu. Kuja kwake mara ya pili kutakuwa wazi, uwezo na sifa kuu na itakuwa ndio mwisho wa uasi na dhambi. Tukio hili litaaadhimisha ufufuo wa wafu na kuzawadiwa kwa watakatifu.
(Mt. Yohana 14:3; Ufunuo 1:7; Matthayo 24:30; 1 Wathesalonike 4:15‐17; Ufunuo 12:10‐12;
Ufunuo 22:12)
Hukumu
Mungu atakuhumu wanadamu wote kupitia kwa Yesu Kristo kama wanawe kupitia kwake. Kwa hali hiyo, wanadamu wote bila juhudi zao wamependwa, wamesamehewa na kushirikishwa ndani ya Yesu ambaye ndiye mfalme na mwokozi wao. Upendo wa Mungu daima hautaisha au kupungua hata kwa wale wanaokataa kukili yeye ni nani kwao, wanakataa upendo wake na kijipeleka jahannamu; hao waasi hawatasherekea matunda ya wokovu ila watashuhudia upendo wake kama hasira/hukumu. Kwa anaowapenda, Mungu huwaadhibu ili wamrejelee na waishi; yeye anasimama kwenye mlango akibisha na kuwaasa waufungulie upendo wake wa milele. Hukumu ya Mungu ndani ya Yesu inamaanisha hatima ya uovu na kufanywa upya kwa dunia na viumbe vyote.
(Matendo ya Mitume 24:15; Mt. Yohana 5:28‐29; Mt. Yohana 3:17; Warumi 5:6; Wakolosai
1:20; 1 Timotheo 2:3‐6; 2 Petro 3:9; Warumi 5:15‐18; Matendo ya Mitume 10:43; Mt. Yohana 12:32; 1 Wakorintho 15:22‐28; Waebrania 12:6; Waefeso 1:10; Ufunuo wa Yohana 3:19‐20)